SADC yaondowa wanajeshi wake Mashariki mwa Kongo
13 Machi 2025Matangazo
Uamuzi wa jumuiya hiyo ya wanachama 16 umepitishwa kwenye mkutano wa kilele, uliokuwa ukijadili juu ya mgogoro huo wa mashariki mwa Kongo,ambao umeshuhudiwa kwa karibu miongo mitatu, ukihusisha machafuko na mauaji ya mamilioni ya watu.
Soma pia:Viongozi wa jumuiya ya SADC kujadili mgogoro wa Kongo
Baada ya mazungumzo yaliyofanyika kwa njia ya mtandao,taarifa ya viongozi wa SADC iliyotolewa ilisema, wamekubaliana kufuta mamlaka ya kikosi cha SAMIDRC ya kuendelea kubakia nchini Kongo na kutowa maelekezo ya kuanza kwa awamu mpango wa kuondoka kwa wanajeshi wa kikosi hicho.
Zaidi ya wanajeshi 12 wa kikosi hicho wameuwawa katika mgogoro wa mashariki mwa Kongo tangua mwezi Januari.