Jumuiya ya maendeleo ya nchi za kanda ya Kusini mwa Afrika SADC imeamua kuondoa wanajeshi wake mashariki mwa Kongo. Uamuzi wa jumuiya hiyo umepitishwa kwenye mkutano wa kilele, uliokuwa ukijadili juu ya mgogoro huo wa mashariki mwa Kongo ambao umeshuhudiwa kwa karibu miongo mitatu. Babu Abdalla amezungumza na mchambuzi wa siasa za Kongo Roger Manzekele akiwa mjini Kinshasa kuhusu uamuzi huo.