Rwanda yawasindikiza wanajeshi wa SADC kuelekea Tanzania
29 Aprili 2025Matangazo
Jeshi la Rwanda linawasindikiza wanajeshi wa vikosi vya jumuiya ya kiuchumi ya kusini mwa Afrika SADC kupitia ardhi yake kwenda Tanzania huku wakiondoka eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Hayo ni kwa mujibu wa msemaji wa jeshi la Rwanda katika kauli yake aliyotoa Jumanne.
Jumuiya ya SADC yenye nchi 16 wanachama ilisema katikati ya mwezi Machi kwamba ilikuwa imefuta mamlaka ya ujumbe wake nchini Kongo, SAMIDRC, na ingeanza kuondoa vikosi vyake kwa awamu kutoka Kongo.
Ujumbe wa SADC ulitumwa Kongo kuisaidia serikali ya mjini Kinshasa kupambana na makundi ya waasi upande wa mashariki mnamo Desemba 2023.