SiasaRwanda
Rwanda yawapokea wahamiaji 7 waliofurushwa Marekani
28 Agosti 2025Matangazo
Hatua hiyo ni sehemu ya mkataba unaoiruhusu Rwanda kuwapokea wahamiaji wanaofurushwa Marekani. Serikali ya Rwanda imesema hayo Alhamisi.
Msemaji wa serikali ya Rwanda Yolande Makolo, ameliambia shirika la Habari la AFP kwamba kundi la kwanza liliwasili Katikati ya mwezi Agosti na kwamba watatu kati yao wamesema wanataka kurudi katika nchi zao.
Lakini wanne wametaka kuishi nchini Rwanda. Maafisa hawakutoa maelezo kuhusu uraia wa wahamiaji hao.
Mnamo Agosti 5, Rwanda ilisema itawakubali wahamiaji 250 kutoka Marekani, na kwamba itakuwa na uwezo wa kumruhusu kila mtu atakayependekezwa kwa ajili ya makazi mapya".