Rwanda yawakamata maafisa watatu wakuu wa sekta ya madini
28 Aprili 2025Ofisi hiyo ya upelelezi, imesema watatu hao ni Augustin Rwomushana, John Kanyangira na Richard Niyongabo wanazuiliwa katika mji mkuu wa Kigali, bila kutaja ni lini walikamatwa.
Ubelgiji: Hatua ya Rwanda mashariki mwa Kongo haziwezi kuhalalishwa
Taarifa ya ofisi hiyo ya uchunguzi imeongeza kuwa maafisa hao watatu walikamatwa pamoja na wafanyabiashara wanne wanaoshukiwa kuhusika katika uhalifu unaohusisha rushwa, matumizi mabaya ya mamlaka kwa kutumia ofisi zao kwa maslahi yao binafsi, kujilimbikizia mali kinyume cha sheria pamoja na utakatishaji fedha .
Mazungumzo ya amani kati ya Kongo na M23 yaahirishwa Doha
Haya yanajiri baada ya Umoja wa Ulaya mwezi Machi kuwawekea vikwazo viongozi wa bodi hiyo, kufuatia hatua ya Rwanda ya kuwaunga mkono waasi wa M23 huko Kongo ili kujipatia madini muhimu.
Haijabainika wazi iwapo maafisa hao wanahusishwa na biashara haramu ya madini kutoka eneo lenye utajiri mkubwa wa rasilimali mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambako Rwandainashutumiwa kuwaunga mkono wapiganaji wanaoipinga serikali ya Kongo kufanya ulanguzi wa madini hayo.