Rwanda yasema bado hakuna mkataba wa amani na Kongo
15 Juni 2025Katika chapisho kwenye mtandao wa kijamii wa X, Nduhungirehe amesema kuwa hafla hiyo haitafanyika leo mjini Washington, Marekani kama ilivyopangwa kwasababu hatua hiyo ya utiaji wa saini inapaswa kuingiliana na uhalisia wa mazungumzo.
Waziri huyo amesema mchakato wa mazungumzo bado unaendelea na kwamba utiaji saini utafanyika mara tu makubaliano ya amani ya ushindi yatakapofikiwa na pande zote.
Rasimu ya amani ya Congo na Rwanda yapokelewa na Marekani
Awali, Nduhungirehe alionya kwamba kuvujisha kwa nia mbaya habari za pande moja kwa vyombo vya habari, kunaweza kuhatarisha mazungumzo.
Haya yanajiri siku chache baada yaRwanda kujiondoa katika jumuiya kuu ya kiuchumi ya Afrika ya Kati, ikishutumu shirika hilo kuegemea upande wa Kongo wakati mapigano yanaendelea.