Rwanda, Marekani zafikia makubaliano kupokea wahamiaji 250
5 Agosti 2025Hayo yanakuja wakati Rais Donald Trump akiongeza makali kwenye kampeni yake ya kukabiliana na uhamiaji nchini mwake.
Makubaliano, ambayo yaliripotiwa kwa mara ya kwanza na shirika la habari la Reuters, yalisainiwa na maafisa waMarekani na Rwanda mjini Kigali mnamo mwezi Juni, kwa mujibu wa chanzo cha ndani ya serikali ya Rwanda.
Chanzo hicho kilisema tayari Washington ilikuwa imeshatuma orodha ya watu kumi wa mwanzo kusafirishwa.
Akihalalisha uamuzi huo wa Kigali, msemaji wa serikali ya Rwanda, Yolande Makolo, alisema nchi hiyo imekubali mpango huo kwa kuwa takribani kila familia nchini humo ina uzoefu wa magumu yanayotakana na ukimbizi.
Trump amepanga kuwahamisha mamilioni ya wahamiaji anaodai wameingia au wanaishi nchini Marekani kwa njia haramu.