MigogoroJamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Rwanda na Kongo zafanya mkutano wa kwanza wa pamoja
1 Agosti 2025Matangazo
Umoja wa Afrika, Qatar na Marekani walihudhuria mkutano huo uliofanyika Washington, ulioanzishwa kama jukwaa la kushughulikia utekelezaji na utatuzi wa migogoro kwenye mkataba huo wa amani.
Katika makubaliano ya Washington, nchi hizo mbili za Afrika ziliahidi kutekeleza mpango wa 2024 ambao ungeshuhudia wanajeshi wa Rwanda wanaondoka mashariki mwa Kongo katika kipindi cha siku 90.
Makubaliano ya mwezi Juni kati ya Rwanda na Kongo yaliashiria mafanikio katika mazungumzo yaliyoratibiwa na serikali ya Rais Donald Trump, yaliyolenga kukomesha mapigano yaliyowaua maelfu ya raia na kuvutia uwekezaji wa magharibi wa mabilioni ya dola katika eneo hilo lenye utajiri wa madini.