Rwanda na DRC kusaini makubaliano ya kumaliza vita
27 Juni 2025Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Marekani, Tommy Pigolt amesema mawaziri wa mambo ya nje wa Kongo na Rwanda watasaini makubaliano hayo mbele ya waziri wa mambo ya nje wa Marekani Marco Rubio.
Nchi hizo tatu zimesema vipengee muhimu kwenye makubaliano hayo ni pamoja na kuheshimu mipaka, kujiepusha na uhasama na kuyapokonya silaha makundi yote yasiyo ya serikali.
Rwanda na DRC waafikiana makubaliano ya awali ya amani
Rais wa Marekani Donald Trump amejisifia mitandaoni kwamba ameendesha juhudi za kidiplomasia za kufikiwa makubaliano hayo, lakini akalalamika kwamba licha ya juhudi zake, kamati ya Nobel ya Norway imekuwa ikipuuza hatua zake za upatanishi katika migogoro mbalimbali.
Amelalamika kwamba kamati hiyo haitotambua juhudi zake kwa kumpa tuzo ya Amani ya Nobel.