Rutte: Trump amejitolea kwa ulinzi wa pande zote NATO
25 Juni 2025"Kwangu mimi, ni wazi kabisa kwamba Marekani imejitolea kabisa kwa NATO, imejitolea kabisa kwa Ibara ya 5. Na, ndiyo kuna pia matarajio ambayo yatatimizwa leo. Tunataka kuhakikisha kuwa sio tu tunaweza kujilinda dhidi ya Urusi na watu wengine lakini pia kuianisha bajeti yetu, alisema Rutte.
Kuna mashaka ya namna utawala huo unavyojitolea katika ulinzi wa washirika wake baada ya taarifa kadhaa kuhoji kuhusu dhamira ya Marekani kwa bara la Ulaya.
Viongozi wa nchi za NATO wakutana The Hague
Awali Trump aliwaambia waandishi habari alipokuwa njiani kuelekea katika mkutano wa kilele wa NATO mjini The Hague Uholanzi, kuna maelezo mengi katika kifungo cha tano cha mkataba unaounda Jumuiya hiyo kinachoeleza kuwa shambulizi dhidi ya nchi moja au zaidi za Ulaya au Amerika ya Kaskazini litachukuliwa kama shambulizi dhidi ya wote.
Trump aliongeza kuwa atafafanua hilo katika mkutano huo na kwamba siku zote anajitolewa kuokoa maisha ya watu.