Rumsfeld aizuru Iraq:
6 Desemba 2003Matangazo
KIRKUK: Waziri wa Mambo ya Ulinzi wa Marekani Donald Rumsfeld ameanza ziara isiyotazamiwa katika mji wa Iraq ya Kaskazini, Kirkuk. Bwana Rumsfeld ana niya ya kuchunguza hali ya kisiasa na wanajeshi wa Kimarekani mjini Kirkuk, alisema msemaji wa serikali ya Marekani. IIisemekana ziara yake hiyo haikutangazwa kutokana na sababu za usalama. Baadaye, Bwana Rumsfeld atakutana mjini Baghdad pamoja na Mtawala wa Mambo ya Kiraiya wa Marekani nchini Iraq, Paul Bremer. Kabla ya hapo, Waziri huyo wa Mambo ya Ulinzi wa Marekani alizizuru Afghnaistan na Georgia.