Rumsfeld aendeleza ziara yake Iraq:
7 Desemba 2003Matangazo
BAGHDAD. Akiendeleza ziara yake nchini Iraq, Waziri wa Mambo ya Ulinzi wa Marekani Donald Rumsfeld amesema anaunga mkono Iraq ikabidhiwe uhuru wake haraka iwezekanavyo. Alipokutana na Naibu wa Waziri Mkuu wa Iraq, Abdel Aziz Hakim, Bwana Rumsfeld alisema ni muhimu yafanyike maendeleo katika swali hilo. Katika hutuba yake iliyoonyeshwa na Shirika la Televisheni ya Iraq AL IRAQIYAH, Bwana Rumsfeld alisisitiza kuwa vikosi vya mwungano vinavyoongozwa na Marekani vitabakia nchini Iraq mpaka limalizike jukumu lao. Mwezi wa Novemba serikali ya Iraq iliwafikiana na Marekani kwamba baada ya kutungwa katiba hapo mwezi wa Februari 2004 vianzishwe vikao vya bunge litakalochaguliwa kutoka makundi yote ya kidini na kikabila. Na hapo mwezi wa Juni serikali ya sasa itateuwa serikali mpya ya mpito. Kufuatana na mipango hiyo uchaguzi wa bunge utafanyika katikati ya Machi mwaka 2005.