Nchini Tanzania chama kikuu cha upinzani CHADEMA kinaonekana kimekumbwa na mpasuko kuhusu sera yao mpya ya "no reform no election" sehemu fulani ya wanachama inaonekana hawakubaliani na sera hiyo. Zaidi juu ya hilo, Mohammed Khelef amezungumza na aliyekuwa katibu wa masuala ya kijamii na kijinsia, Catherine Ruge.