Rubio na Ruto watoa wito wa kusitishwa kwa mapigano Kongo
22 Februari 2025Matangazo
Katika taarifa, msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Marekani Tammy Bruce, amesema wawili hao walisisitiza kwamba hakuna suluhisho la kijeshi katika mzozo kati ya jeshi la serikali la Kongo na waasi wa M23.
Marekani yamuekea vikwazo afisa wa Rwanda na msemaji wa M23
Taarifa hiyo pia imesema viongozi hao wawili wamesisitiza kujitolea kwao kushinikiza utatuzi wa mzozo huo kwa njia ya kidiplomasia.
Baraza la Usalama la UN latoa wito kwa Rwanda kuacha kuwaunga mkono waasi wa M23
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa mara ya kwanza limetoa wito kwa Rwanda kuacha kuwaunga mkono waasi wa M23 na kumaliza umwagaji damu. Baraza hilo limetoa wito huo wakati waasi hao wakizidi kusonga mbele katika maeneo kadhaa mashariki mwa Kongo.