Rubio na Lavrov wazungumza kabla ya mkutano wa Alaska
13 Agosti 2025Matangazo
Viongozi hao wawili kwa pamoja wameelezea matumaini yao kwamba waliyoyajadili yatafanikiwa, bila hata hivyo kutoa maelezo zaidi.
Aidha, mkutano kati ya rais wa Marekani Donald Trump na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin utafanyika siku ya Ijumaa katika mji wa Anchorage jimboni Alaska. Hayo yameelezwa na Msemaji wa Ikulu ya White House Karoline Levitt aliyeongeza kuwa Trump ataelekea huko Anchorage Ijumaa asubuhi.
Leavitt amesema kufikia muda huu, hakuna ratiba yoyote iliyotangazwa kwa kuwa hilo bado linajadiliwa na pande zote, lakini akathibitisha kuwa viongozi hao wawili wamepanga kuwa na mazungumzo ya moja kwa moja kuhusu namna ya kuvimaliza vita vya Ukraine.