Rubio: Matumaini ya amani Ukraine ni madogo mno
16 Mei 2025Matangazo
Katika ujumbe wa video alioutoa kupitia mtandao wa kijamii wa Telegram, Medinsky amesema wako tayari kufanya kazi na kwamba hapo jana Alhamis walikuwa na mazungumzo mazuri na waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Hakan Fidan.
Kwa upande wake Ukraine kupitia Rais Volodymyr Zelenskiy imesema, inautuma ujumbe wake unaoongozwa na waziri wa ulinzi Rustem Umerov, licha ya kuwa ujumbe wa Moscow haujumuishi yeyote anayefanya maamuzi kuhusiana na vita vya Ukraine.
Haya yanafanyika wakati ambapo waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Marco Rubio amesema matumaini ni madogo mno kwa mazungumzo hayo ya amani kutoa mwafaka, baada ya pande hizo mbili kushambuliana kwa maneno kuelekea mazungumzo hayo.