Rubio: Marekani haitoiwekea Urusi vikwazo zaidi kwa sasa
25 Juni 2025Matangazo
Rubio amesema iwapo Marekani itafanya kile kila mtu anachotaka ifanye ambacho ni kuiwekea Urusi vikwazo zaidi basi watapooteza nafasi ya kuzungumza akisisitiza kuwa rais Donald Trump atajua muda na wakati muafaka wa kuchukua hatua za kiuchumi dhidi ya Urusi.
Rubio ameongeza kuwa Marekani itaitumia nafasi yoyote ya kubadilisha hali ili ifanikiwe kufikia makubaliano ya amani kati ya Urusi na Ukraine.
Watu takriban 18 wauwawa Ukraine
Viongozi wa nchi za Jumuiya ya kijeshi ya NATO wamekusanyika huko Uholanzi kushiriki kwenye mkutano huo ambao mada kuu ni juu ya wanachama kuongeza fedha katika bajeti ya ulinzi hadi asilimia 5 ya Pato la Taifa, ingawa baadhi ya wanachama wanapinga hatua hiyo.