SiasaAsia
Rubio kukutana na Lavrov kando ya mkutano wa ASEAN, Malaysia
10 Julai 2025Matangazo
Viongozi hao watakutana kando ya mkutano wa mawaziri wa mambo wa kigeni wa Jumuiya ya ushirikiano wa kiuchumi na kiusalama ya nchi za Kusini Mashariki mwa Asia, ASEAN unaofanyika katika mji mkuu wa Malaysia, Kuala Lumpur.
Huu utakuwa ni mkutano wa pili wa ana kwa ana kati ya Rubio na Lavrov, na unajiri wakati vita vya Ukraine vikiendelea kupamba moto huku rais wa Marekani Donald Trump akionekana kuchukizwa na hatua za rais wa Urusi Vladimir Putin.
Mkutano wa kwanza kati ya wanadiplomasia hao wakuu ulifanyika Saudi Arabia mwezi Februari kama sehemu ya juhudi za utawala wa Trump za kuanzisha upya mahusiano baina ya Marekani na Urusi kujaribu kuvimaliza vita vya Ukraine.