Rubio awasili Jerusalem kwa mkutano na Netanyahu
16 Februari 2025Matangazo
Akiwa nchini Israel Rubio anatarajiwa kushinikiza pendekezo la rais wa Marekani Donald Trump linalopingwa na wengi la kuchukua udhibiti waUkanda wa Gaza na kuwahamisha wakaazi wake zaidi ya milioni 2 katika mataifa mengine.
Awali kundi la Hamas limesema kauli hiyo ya Trump ni uchokozi dhidi ya watu wa Gaza na mpango huo hautakuwa na faida yoyote katika kuleta utulivu na uthabiti wa kanda ya Mashariki ya Kati.
Sintofahamu kuhusu hatma ya mpango wa usitishwaji mapigano Gaza
Ujerumani nayo ilisema watu wa Palestina hawapaswi kuhamishwa kutoka Ukanda wa Gaza, na kwamba eneo hilo halitakiwi kukaliwa au kutawaliwa tena na Israel.