Rubio akanusha kuwa Utawala wa Trump unaupendelea Urusi
21 Februari 2025Rubio amesema Marekani inataka kwanza kuona kama Urusi imejitolea katika mazungumzo hayo.
Katika mahojiano yaliochapishwa jana kwenye mtandao wa kijamii wa X, Rubio alisema kuwa Trump anataka vita hivyo kumalizika na kuongeza kwamba pia anataka kujuwa kama Urusi imejitolea katika kumaliza vita hivyo.
Rubio amesema haungi mkono mengi yaliofanywa na rais wa Urusi Vladimir Putin ila hatimaye wanapaswa kuwa na uwezo wa kuzungumza na taifa ambalo, katika baadhi ya matukio, lina hifadhi kubwa zaidi ya mbinu za nyuklia duniani, na ya pili kwa ukubwa, ikiwa sio kubwa zaidi, yenye hifadhi ya silaha za kimkakati za nyuklia duniani.
Suala la Ukraine latawala mkutano wa mawaziri wa nje wa G20
Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema kuwa Rubio na mwenzake wa Urusi Sergei Lavrov walikubaliana mjini Riyadh, Saudi Arabia kuteuwa timu za ngazi ya juu kuanza kufanyia kazi njia ya kumaliza mzozo wa Ukraine haraka iwezekanavyo.