Rubio afanya ziara Umoja wa Falme za Kiarabu
19 Februari 2025Matangazo
Baada ya kuwasili Abu Dhabi asubuhi, mwanadiplomasia huyo mkuu wa Marekani anatarajiwa kukutana na Rais wa Umoja huo wa Falme za Kiarabu Mohammed bin Zayed Al Nahyan pamoja na waziri wa mambo ya nje Abdullah bin Zayed Al Nahyan.
Soma zaidi:Ziara ya Rubio: Netanyahu asifu msimamo wa Trump kuhusu Gaza
Hapo jana, Rubio aliongoza ujumbe wa Marekani katika mazungumzo ya nadra na maafisa wa Urusi walioongozwa na waziri wa mambo ya nje Sergei Lavrov katika mji mkuu wa Saudi Arabia.
Majadiliano hayo yalihusu masuala mbalimbali, ikiwa ni pamoja na juhudi za kumaliza vita nchini Ukraine.