Rubio aelekea Ulaya kwa mkutano na mawaziri wa NATO
2 Aprili 2025Rubio atashiriki mkutano huo katika wakati ambapo hali ya wasiwasi inazidi kuongezeka kati ya mataifa ya Ulaya na Marekani, Rais Donald Trump akiweka ushuru dhidi ya mataifa ya Ulaya pamoja na kupinga uhuru wa Denmark juu ya eneo lake linalojitawala la Greenland.
Mazungumzo na maandalizi ya mkutano wa kilele The Hague
Mazungumzo hayo ya siku mbili ni maandalizi ya mkutano wa kilele wa viongozi hao utakaofanyika Juni mjini The Hague.
Rasmussen asema Denmark haijafurahishwa na matamshi ya Vance
Waziri wa mambo ya nje wa Denmark Lars Lokke Rasmussen, anayetarajia kukutana na Rubio mjini Brussels, amesema nchi yake haikufurahishwa na kauli ya makamu wa Rais wa Marekani JD Vance wakati wa ziara yake wiki iliyopita katika kambi ya kijeshi ya Marekani huko Greenland,ambapo alisema kuwa Denmark haijawatendea vyema watu wa eneo hilo la Greenland.