Wapiganaji wa RSF waishambulia kambi ya wakimbizi ya Zamzam
15 Februari 2025Wapiganaji hao wa RSF wanajaribu kuimarisha ngome yao huko Darfur huku ikipoteza udhibiti katika mji mkuu, Khartoum.
Mapigano ya hivi karibuni yameendelea kuiweka Sudan katika hali mbaya zaidi wakati ambapo nusu ya idadi ya watu wa Sudan wametumbukia kwenye baa la njaa, huku mamilioni ya wengine wakiwa wakimbizi tangu Aprili mwaka 2023.
Soma pia: Mgogoro wa Sudan: Vizuizi vya misaada, njaa na mpango wa utawala wa kiraia
Shirika la madaktari wasio na mipaka MSF limethibitisha vifo vya watu saba kufuatia mashambulizi hayo ya hivi karibuni katika kambi hiyo huku wakaazi wa eneo hilo wakisema huenda idadi ya waliokufa ikawa juu zaidi.
Shirika hilo limeongeza kwamba mashambulizi haya yamewapa wakati mgumu madaktari wake kufanya shughuli zao katika kambi ya Zamzam. Shirika la Kimataifa la Uhamiaji linasema kambi ya zamzam ina zaidi ya wakimbizi milioni moja waliokimbia vita vinavoendelea nchini Sudan.