Ronaldo atimiza miaka 40 akiwa na mafanikio tele kisoka
5 Februari 2025Rekodi za dunia alizozivunja
- Ronaldo ana mabao mengi zaidi katika soka la kimataifa la wanaume akiwa na 135. Aliivunja rekodi ya awali ya Ali Daei wa Iran ya magoli 108 mnamo mwezi Juni 2021.
- Ronaldo (135), Lionel Messi (112) na Daei (108) ndio watu pekee wenye magoli zaidi ya mia moja ya kimataifa wakati Ronaldo pekee amecheza mechi 200 na timu yake ya taifa.
-Kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya ama Champions League pia, Ronaldo anashikilia rekodi mbili za magoli 141 na kucheza mara 187.
- Ronaldo alikuwa ni mchezaji wa kwanza kufikisha magoli 100, katika kipindi cha mwaka mmoja tu, kabla ya kuibuka mpinzani wake Messi, ingawa Messi alifikisha idadi hiyo katika mechi 123, huku Ronaldo akifikisha baada ya kucheza mechi 137.
- Ronaldo ni mchezaji pekee aliyefunga katika mechi tatu za fainali za Michuano ya Mabingwa Ulaya, lakini pia anashikilia rekodi ya kufunga magoli 17 kwenye msimu wa michuano hiyo wa (2013-14) na kufunga kwenye mechi 11 alizocheza.
- Ana magoli 10 dhidi ya Juventus, hii ikiwa ni idadi kubwa ya magoli kwenye michuano ya Mabingwa kuwahi kufungwa na mchezaji yoyote dhidi ya mpinzani mmoja.
- Messi ana magoli 129 na Robert Lewandowski akiwa mchezaji pekee mwingine aliyefikia idadi ya zaidi ya magoli mia moja (103) kwa msimu huu.
Real Madrid
- Ronaldo ndiye mfungaji bora wa Real Madrid akiwa na mabao 450, ambayo ni karibu na magoli 100 dhidi ya Karim Benzema (354) aliyeshika nafasi ya pili.
Soma pia:Ronaldo akasirishwa kunyang'anywa taji na Modric
- Alifunga mabao hayo katika mechi 438, hivyo kumpa uwiano bora zaidi kuliko ule wa bao kwa kila mchezo na wastani wa mabao 50 katika kila msimu, miongoni mwa 9 aliyocheza.
- Alifunga mabao 61 katika mashindano yote 2014-15 na magoli 60 katika msimu wa 2011-12.
Manchester United
- Ronaldo alifunga mabao 118 katika kipindi chake cha kwanza akiwa na Manchester United, baada ya kutokea Sporting Lisbon mwaka 2003 na kuondoka kwenda Real Madrid, akinunuliwa kwa kiasi kikubwa cha fedha kilichovunja rekodi wakati huo cha pauni milioni 80 (dola milioni 100) mnamo 2009.
- Alirejea Manchester United muongo mmoja baadaye mnamo 2021, na kufunga mabao 24 katika msimu wake wa kwanza, na kisha mengine matatu kabla ya kuondoka tena katikati ya sintofahamu mnamo Disemba 2022.
- Msimu wenye mafanikio zaidi kwa Ronaldo akiwa na United ulikuwa ni wa 2007-08, ambapo alishinda Kiatu cha Dhahabu cha Ligi ya Premier akiwa na mabao 31 na mabao 42 kwenye mashindano yote.
Tuzo
- Ronaldo ameshinda rekodi ya mataji matano ya Ligi ya Mabingwa, manne akiwa na Real baada ya kushinda kwa mara ya kwanza akiwa na Manchester United mwaka 2008.
- Ameshinda Ballon d'Or, tuzo ya mchezaji bora wa dunia, mara tano - Ni nyota wa Argentina tu Lionel Messi aliyemzidi kwa kushinda mara nane tuzo hiyo. Alitunukiwa tuzo maalum ya mafanikio bora ya kazi yake katika Tuzo za Ubora za FIFA za 2021.
- Akiwa na Real Madrid Ronaldo pia alishinda mataji mawili ya LaLiga, Copa del Rey, Supercopa de Espana na UEFA Super Cup na Makombe Matatu ya Dunia ya Vilabu.
- Akiwa na United alishinda mataji matatu ya Ligi Kuu, Kombe la FA, mawili Kombe la Ligi, Ngao ya Jamii na Kombe la Dunia la Klabu.
- Mataji mawili ya Serie A na Juventus yalimfanya nyota huyo kuwa na mataji saba ya ligi.
- Makombe mengine ni pamoja na Euro 2016 na Ligi ya Mataifa ya 2018-19 akiwa na Ureno, Kombe la Ureno la Super Cup akiwa na Sporting na Arab Club Champions Cup akiwa na timu ya Saudi Al Nassr.
- Ronaldo ameshinda Kiatu cha Dhahabu cha Ulaya mara nne na alikuwa mfungaji bora wa Euro 2020. Amefunga mabao 923 katika maisha yake yote katika mechi 1,263 alizocheza.