ROME:Mtuhumiwa kurudishwa Uingereza
18 Agosti 2005Matangazo
Italia imeidhinisha hatua ya kurudishwa nchini Uingereza kwa Osman Hussein anaetuhumiwa kuhusika na mashambulio viza yaliyofanyika mjini London mwezi uliopita.
Bwana Hussein ambae pia anaitwa Hamdi Isaac alikamatwa mjini Rome siku chache baada ya mashambulio hayo.
Mahakama husika, imesema itamkabidhi mtuhumiwa huyo kwa Uingereza mnamo muda wa siku 35 zijazo.
Mawakili wake wana muda wa siku kumi wa kukata rufani ili kupinga uamuzi wa mahakama .
.