Rome:Khofu yazidi kutanda katika usafiri wa ndege nchini Uingereza.
18 Agosti 2006Matangazo
Ndege ya abiria ya Uingereza chapa boing 767 ilyokuwa njiani kuelekea Misri imetua kwa ghafla hii leo katika uwanja wa ndege wa Brindisi kusini mwa Italy.
Shirika la habari la Italy ANSA linasema, ndege hiyo imetua kutokana na onyo la kuwepo bomu ndani yake.
Idara za usalama kutoka uwanja wa ndege huo zimesema, abiria wameshateremshwa kutoka ndani ya ndege hiyo, na polisi wanaopambana na ugaidi wanaikagua.