Romania na Bulgaria zaingia rasmi katika eneo la Schengen
1 Januari 2025Katika eneo la Kulata kwenye mpaka na Ugiriki, Waziri Mkuu wa Bulgaria Dimitar Glavchev, ameitaja hatua ya nchi yake kuwa mwanachama kamili wa eneo la Schengen kama "tukio la kihistoria."
Sherehe ya kuondolewa kwa vizuizi vya ukaguzi wa mipaka kati ya Romania na Bulgaria ilifanyika katika kivuko cha mpakani cha Giurgiu-Russe ambapo mawaziri wa mambo ya ndani wa nchi hizo mbili walihudhuria.
Soma pia: Je, ongezeko la udhibiti wa mipaka ya ndani linaua ndoto ya EU?
Kwa Romania na Bulgaria kujiunga na Schengen kunalifanya eneo hilo kuwa na nchi wanachama 29, ikijumuisha mataifa mengi ya Umoja wa Ulaya pamoja na Uswisi, Norway, Iceland na Liechtenstein ambazo sio nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya EU.
Hata hivyo, nchi kadhaa – ikiwemo Ujerumani – hivi karibuni zimeanzisha tena ukaguzi mipakani kama sehemu za kupambana na uhamiaji haramu.