RIYADH: Washukiwa wawili wa ugaidi wauwawa Saudi Arabia.
4 Aprili 2005Matangazo
Wanajeshi wa Saudi Arabia wamewauwa washukiwa watatu wa ugaidi waliokuwa wa mejifungia kwenye nyumba moja katika mji wa Al- Ras kilomita 300 kaskazini mwa Riyadh.
Gavana wa mkoa Al Qassim ameviambia vyombo vya habari kuwa watu wengine wawili waliokuwa wakitafutwa na polisi waliumizwa vibaya katika shambulio hilo la kufyatuliana risasi.
Mwana wa Mfalme Faisal bin Bandar bin Abdel Aziz amesema kuwa malumbano hayo yalichukua takriban masaa 12.
Katika miaka miwili ya mapambano dhidi ya ugaidi zaidi ya raia 90 na askari 39 wameauwawa Saudi Arabia kufikia sasa kutokana na visa vya mashambulizi kutoka kwa wafuasi wa Al Qaeda kundi linalo ongozwa na Osama bin Laden.