RIYADH: Ubalozi wa Marekani nchini Saudi Arabia kufungwa
8 Agosti 2005Matangazo
Ubalozi mdogo wa Marekani mjini Riyadh nchini Saudi Arabia utafungwa hii leo na hapo kesho kufuatia vitisho vya mashambulio dhidi ya majengo ya Marekani. Serikali ya Saudi imesema haina habari zozote kuhusiana na njama ya mashambulio katika ufalme huo.
Taarifa ya Marekani imesema ubalozi wake mjini Riyadh na balozi ndogo mjini Jedah katika bahari ya Shamu na mji wa Dhahran mashariki mwa nchi hiyo zitafungwa. Raia wa Marekani wanaoishi Saudia wameonywa wawe waangalifu.